Ijumaa 1 Agosti 2025 - 23:56
Lengo la Shambulio la Moja kwa Moja Dhidi ya Iran Lilikuwa Kutekeleza Mradi wa “Kufutwa Ustaarabu”

Hawza/ Ayatollah Kaabi alisema: Mpango wa kusitisha vita ni dhaifu, Ikiwa utawala wa Kizayuni na Marekani wakichukua hatua tena, taifa la Iran litajibu kwa nguvu zaidi kuliko hapo awali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, likinukuu kutoka kwenye tovuti ya habari ya Miftah ya Sayansi za Kibinadamu za Kiislamu, kufuatia matukio muhimu na ya kihistoria ya vita vya siku 12, Ayatollah Abbas Kaabi, mwanachama wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, alichambua vipengele vya kiutamaduni, kijamii na kistratejia vya tukio hili, na matini kamili ni kama ifuatavyo:

الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلا على خير الأنام، المصطفى ابوالقاسم محمد وعلى آله الطيبين الطاهرين، لا سيما بقية الله في الأرضين

Vita ya siku 12 ambayo utawala wa Kizayuni uliilazimisha Iran, kwa hakika inapaswa kuitwa “Ulinzi Mtakatifu wa Pili.” Tukio hili, mbali na funzo na maonyo mengi, lilikuwa na mafanikio ya kimaada na ya kiroho kwa taifa la Iran. Ikiwa tutathamini mafanikio haya na kuyahifadhi, mfumo wa Kiislamu utaendelea na njia yake ya ukuaji wa kasi, katika pande zote mbili za kimaada na kiroho, hadi kufikia kiwango cha nguvu mpya ya kistaarabu.

Vita hii ilikuwa na sura nyingi, moja kati ya muhimu zaidi ikiwa ni kulinda umoja wa kitaifa. Ushiriki wa pamoja na wa kuvutia wa taifa la Iran katika uwanja—kwa mitazamo yote, mielekeo, makabila na mitiririko ya kisiasa—ulikuwa ishara dhahiri ya umoja wa kitaifa, kwa taifa liitwalo Iran, kiwango hiki cha mshikamano ni kuibuka na kudhihiri kwa umoja wa kistaarabu. Taifa la Iran, kwa kutegemea historia yake ya kale, utajiri wake wa kitamaduni na mtaji wake wa kijamii, kwa mara nyingine tena liliweka wazi kwamba linakuwa na mshikamano linapokabiliana na wageni.

Hisia za jumla za watu zilikuwa kwamba Marekani na Uzayuni wa kimataifa walitaka kupora mali za kistaarabu za Iran na kuteka historia, utamaduni na utambulisho wa taifa hili. Katika kujibu tishio hili, taifa la Iran iliinuka; iliinuka kulinda utambulisho, heshima na ukubwa wake. Ulinzi huu ulikuwa ulinzi wa kistaarabu; ulinzi wa kurejesha utambulisho wa kina wa kitaifa na kidini, na hili si jambo linaloweza kupuuzwa kirahisi kutokana na tukio hili, vitabu kadhaa vinaweza kuandikwa.

Hapa ninagusia tu mambo machache ninayoona ni muhimu sana. Vita hivi, mbali na vipengele vyake vingine, vilikuwa na kipengele muhimu cha kistaarabu, Taifa la Iran lilidhihirisha asili yake ya kimaumbile. Katika kipindi cha miaka 46 iliyopita, Marekani na Uzayuni wa kimataifa wamejaribu chaguo mbalimbali dhidi ya taifa la Iran; bila shaka hata kabla ya Mapinduzi haya jitihada zilikuwepo, lakini baada ya Mapinduzi zikawa kali zaidi na za wazi zaidi.

Chaguo la kwanza lilikuwa “umeng’enyaji wa kistaarabu”; walidhani wanaweza kuliyeyusha taifa la Iran, ambalo lilikuwa limeanzisha mapinduzi mapya, ndani ya ustaarabu wa Magharibi na kulifanya likubalike nalo. Lakini taifa la Iran, kwa mwongozo wa Imam mwanzilishi wa Mapinduzi na baada yake Kiongozi Mkuu wa sasa, kwa uthabiti lilitangaza kwamba sisi ni taifa lenye ustaarabu na tunataka kufufua ustaarabu wetu. Tunataka uhuru, maendeleo, heshima, hadhi, kustahimilika, ujasiri na kujenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe.

Waliposhindwa katika mradi huu wa “kuharibu ustaarabu”, walielekea katika chaguo la pili: “kuzuia kwa ustaarabu.” Walijaribu kuzuia kuenea kwa ustaarabu uliotokana na Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo na duniani; kupitia vizuizi vya pande mbili na sera mbalimbali. Lakini pia hapa walishindwa. Kwa sababu kambi iitwayo “mhimu wa upinzani wa Kiislamu” iliundwa. Mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu—mtazamo wa uhuru, maendeleo, heshima, hadhi na upinzani wa mataifa—uliendelea kuenea. Uamsho wa Kiislamu ulijitokeza, roho ya heshima na uhuru ikaongezeka, na serikali nyingi za kikabaila katika eneo hili zikaanguka moja baada ya nyingine.

Ustaarabu wa Kiislamu, uliotokana na mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu, ulijitokeza kama ukweli katika kiwango cha mahusiano ya kimataifa. Mradi wa kuzuia ustaarabu—si kwa vita vya kijeshi, si kwa vita vya kiuchumi, wala kwa vita vya kiutambuzi—haukuzaa matunda.

Baada ya kushindwa katika miradi ya “uharibifu wa ustaarabu” na “kuzuia ustaarabu”, maadui waliingia katika awamu ya tatu: ufutaji wa ustaarabu.
Katika hatua hii, walilazimika kukimbilia vita vya moja kwa moja, na kwa muktadha huu, walibuni mradi wa Daesh. Lengo la kuunda Daesh halikuwa tu kuleta machafuko, bali kufuta matunda ya ustaarabu ya Mapinduzi ya Kiislamu, kuleta mgawanyiko kati ya umma wa Kiislamu, na kuunda wapinzani wa uongo na viongozi bandia katika ulimwengu wa Kiislamu.

Lakini kwa kuibuka kwa "ushujaa wa ulinzi wa haram", Daesh ilifutwa kabisa. Hii pia ilionyesha kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yana nguvu ya kudumu ya kistaarabu. Kisha, kwa kutokea kwa "Kimbunga cha al-Aqsa", nguvu ya kistaarabu ya upinzani wa Kiislamu ilionyeshwa tena. Operesheni hii ilileta kushindwa kwa uzito mkubwa kwa utawala wa Kizayuni na ustaarabu wa Magharibi, kwa upande wa kijasusi, kiusalama, kijeshi, kisiasa na kiheshima.

Katika wiki zile za mwanzo, Netanyahu alitamka wazi kwamba kushindwa kwa Israeli ni sawa na kushindwa kwa ustaarabu wa Magharibi, kwa sababu wao wanaiona Israeli kama kambi ya mstari wa mbele ya ustaarabu wa Magharibi. Kimbunga cha al-Aqsa kwa hakika kilikuwa ni kiwango cha mabadiliko ya kistaarabu. Sio tu kwamba Mapinduzi ya Kiislamu hayakushindwa, bali yalikua na misingi yake ya kistaarabu ikawa imara zaidi.

Sasa yapata karibu miaka miwili tangu Kimbunga cha al-Aqsa. Licha ya kutokuwepo kwa sura kama za shahidi Haj Qasem Soleimani na shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, na pia utawala wa mitiririko ya kujisalimisha na isiyo na basira nchini Syria ambayo iliwekwa chini ya udhibiti wa kambi ya Magharibi, Mapinduzi ya Kiislamu bado yanaendelea na njia yake ya kistaarabu.

Wengi wa wale walioko madarakani katika baadhi ya nchi kwa sasa, ama kwa ujinga wamepotoshwa, au kwa miaka mingi wamekuwa ni vibaraka wa Magharibi. Maadui baada ya kushindwa katika vita vya kiakili na mzingiro wa kiuchumi, walifikia hitimisho kwamba lazima washambulie moja kwa moja ndani ya taifa la Iran na kufikisha mradi wa kufutwa kwa ustaarabu katika kilele chake.

Kwa dhana kwamba Iran ipo katika hali dhaifu kabisa, walijaribu kwa shambulio gumu na la ghafla, kuvunja ndani Mapinduzi ya Kiislamu; walilenga makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia na kuwaua watu wanyonge wa Iran.

Lakini Iran, kutokana na asili yake yenye mizizi ya kina ya ustaarabu, ilirejesha nguvu mara moja. Taifa la Iran liliingia uwanjani na likafanya mashambulizi ya kihistoria na ya kusifiwa; mashambulizi ambayo moja ya taswira zake za kung’aa ilikuwa umoja wa kitaifa na mshikamano wa kijamii. Umoja huu, sambamba na uwezo wa makombora na mipango ya busara ya uongozi iliyorejesha utulivu na mshikamano nchini, yalisababisha utawala wa Kizayuni kushindwa kwa kishindo na kuomba usitishaji vita.

Hata hivyo, usitishaji huu wa vita ni dhaifu. Ikiwa utawala wa Kizayuni na Marekani wakichukua hatua tena, taifa la Iran litajibu kwa nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa awali, Kulingana na kanuni ya Qur’ani:

“وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا”
“Mkirejea, nasi tutarejea”

Inatarajiwa kwamba maadui katika hatua zijazo wataweka mkazo wao katika kuvunja mshikamano wa kitaifa wa Iran. Ikiwa tutaweza kulinda mshikamano huu wa kitaifa, unaotegemea utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu, maadui hawataweza kufanya chochote.

Mfano wa dhihirisho la mshikamano huu ni wimbo wa “Ey Iran” ulioimbwa na Haj Mahmoud Karimi na kupokelewa kwa furaha na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi. Wimbo huu ni ishara ya kurejeshwa kwa utambulisho wa kijamii na wa kistaarabu wa taifa la Iran; utambulisho uliojengwa juu ya tauhidi, uadilifu na heshima ya binadamu.
Iran yetu, Iran ya Mwenyezi Mungu, ya Ashura na ya Imam Ridha, ni Iran yenye muungano wa kina kati ya Iran na Uislamu, muungano wa kistaarabu usiotenganishwa.

Lakini adui anajaribu kuunda mgawanyiko kati ya Iran na Ashura, kati ya Iran na asili yake ya kistaarabu. Tunapaswa kusimama kwa umakini kamili dhidi ya migawanyiko hii. Baadhi ya migawanyiko ambayo adui anaweza kufuata ni pamoja na:

1- Mgawanyiko kati ya Iran na Uislamu;
2- Mgawanyiko kati ya viongozi na wananchi wa kawaida;
3- Na muhimu zaidi: kughafilika juu ya adui na mipango yake.

Hatuwezi kuangukia katika mtego wa migawanyiko hii. Ni lazima tulinde umoja na mshikamano wa kitaifa kwa mtazamo wa kistaarabu, ustaarabu wa Iran si ustaarabu unaoweza kufutwa; ni hai, imara na leo katika kiwango cha mahusiano ya kimataifa, inajitokeza kama nguvu mpya ya kistaarabu.

Sote, iwe viongozi au wananchi, lazima kwa mujibu wa amri saba za uongozi, tutimize majukumu yetu ya kulinda nguvu hii ya kistaarabu, amri hizi kwa hakika ni mgawanyo wa majukumu kwa ajili ya kuthibitisha na kuendeleza ustaarabu wa Kiislamu:

1- Taifa lazima lilinde mshikamano na umoja;
2- Vikosi vya kijeshi lazima vilinde usalama, uhuru na nguvu ya kijeshi;
3- Chuo cha dini na uongozi wa kidini lazima viwe na jukumu la kuongoza kiroho, kuimarisha subira na ustahimilivu, na kuleta utulivu na nuru.

Hatimaye, inapaswa kusemwa kwamba pigo ambalo utawala wa Kizayuni umepokea kutoka kwa uasi wa kistaarabu wa taifa la Iran, ni kubwa na lenye kuumiza zaidi kuliko mapigo ya makombora.

Ushindi dhidi ya kambi ya uistikbari wa dunia unahitaji mkusanyiko wa sababu na mambo ya msingi. Miongoni mwa sababu hizi ni pamoja na hekima na mipango ya uongozi ambayo ina jukumu muhimu katika kuelekeza harakati ya kitaifa. Vilevile, mwongozo na nuru ambavyo vipo chini ya jukumu la chuo cha dini na uongozi wa kidini, vina umuhimu mkubwa katika kuimarisha kipengele cha kiroho cha jamii na kuleta utulivu na subira kwa watu. Sambamba na haya, kueneza mtazamo wa “kueneana huruma kati yao” kwa ajili ya kuongeza mshikamano na ushirikiano wa kitaifa, ni lazima. Hatimaye, viongozi na maafisa wanapaswa kwa kuamsha mstari wa huduma, waimarishe ufanisi wa mfumo na kuchukua hatua katika kutatua matatizo ya watu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha